JAKARTA:20 wafa kutokana na mafuriko Indonesia
5 Februari 2007Matangazo
Watu 20 wamekufa kutokana na mafuriko katika mji mkuu wa Indonesia, JAKARTA na watu wengine laki 3 na alfu 40 wamepoteza makao yao.
Maafisa wa nchi hiyo wamesema kuwa mafuriko makubwa kama hayo hayajawahi kutokea katika kipindi cha miaka mitano iiyopita nchini Indonesia. Maji yalifikia urefu wa mita 4 katika baadhi ya sehemu za mji.
Watabiri wa hali ya hewa wametahadhrisha kuwa mvua nyingine kubwa zinaweza kuendelea kwa muda wa wiki nzima ijayo.