1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL.Papa akutana na kiongozi wa kanisa la Orthodox

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoD

Baba mtakatifu Benedikt wa 16 katika ziara yake nchini Uturuki amekutana na kiongozi wa kanisa la Greek Orthodox Bartholomew wa kwanza katika mji wa Istanbul.

Ziara ya baba mtakatifu ina lengo la kuziba ufa baina ya kanisa hilo lililo jitenga kutoka kanisa katoliki takriban mika 1000 iliyopita.

Licha ya kuwepo waumini wachache wa kanisa hilo mjini Istanbul Bartholomew bado anatambuliwa miongoni mwa viongozi wa kwanza wa kanisa hilo la Orthodox.