ISTANBUL: Maelfu ya watu watoa heshima zao za mwisho kwa mwandishi wa habari | Habari za Ulimwengu | DW | 23.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISTANBUL: Maelfu ya watu watoa heshima zao za mwisho kwa mwandishi wa habari

Maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa kidini wa Armenia na wanadiplomasia wa kigeni wamekusanyika mjini Istanbul kutoa heshima zao za mwisho kwa mwandishi wa habari raia wa Uturuki mwenye asili ya kiarmenia, Hrant Dink.

Dink aliuwawa kwa kupigwa risasi na kijana wa miaka 17 mwenye siasa kali za kizalendo.

Wakiwa wamevaa mavazi meusi waombolezaji walikusanyika nje ya ofisi za gazeti la Agos ambako Dink alipigwa risasi mara tatu Ijumaa mchana wiki iliyopita.

Dink atazikwa katika makaburi ya Waarmenia baada ya ibada nje ya ofisi ya gazeti alilolianzisha.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com