1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Mlipuko karibu na Lal Masjid

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBef

Mlipuko mkubwa umetokea kwenye hoteli moja karibu na msikiti wa Lal mjini Islamabad na kusababisha vifo vya polisi 13 na kujeruhi wengine 50.Picha za televisheni zinaonyehsa miili iliyoteketea na kurowa damu.Kwa mujibu wa mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo Amir Mehmood,mlipuko ulitokea kwenye mkahawa wa Muzaffar ulio sokoni.Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha mlipuko huo.Eneo hilo ndiko kulikotokea ghasia pale waislamu walio na msimamo mkali walipoteka msikiti mwekundu na kuvamiwa na jeshi la Pakistan.Waandamanaji wanaripotiw akuondoa matofali waliyotumia kuziba barabara ya kuelekea kwenye msikiti ili kuzipa nafasi ambulensi.