ISLAMABAD : Mvulana ajiripuwa na kuuwa watu 18 | Habari za Ulimwengu | DW | 11.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Mvulana ajiripuwa na kuuwa watu 18

Mshambuliaji wa kujitolea muhanga mwenye umri kati ya miaka 15 amejiripuwa na kibasi kiogo kilichokuwa kimejaa watu kaskazini magharibi mwa Pakistan leo hii na kuuwa watu 18.

Mvulana huyo aliripuwa mabomu aliyokuwa amejipachika mwilini wakati wanausalama walipomtaka asimamishe gari na kujisalimisha katika mji wa Dera Ismail Khann.

Maafisa wawili wa polisi, wanajeshi wawili na abiria waliuwawa kutokana na mripuko huo ambao umejeruhi watu 24.

Pakistan imekabiliwa na mashambulizi kadhaa tokea vikosi vya usalama kuuvamia Msikiti Mwekundu wa itikadi kali mjini Islamabad hapo mwezi wa Julai ambapo watu 250 waliuwawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com