1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Musharraf na Bhuto wafikia maridhiano

5 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7ID

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan bibi Benazir Bhuto na rais Pervez Musharraf wamefikia maridhiano.

Mapatano hayo yatamwondolea mwanasiasa huyo mashtaka ya rushwa yanayomkabili, aidha ataweza kushiriki katika uongozi pamoja na rais Musharraf hatua ambayo inatazamiwa kumaliza mvutano wa kisiasa nchini Pakistan.

Bibi Bhuto amepanga kurejea nchini humo katika wiki mbili zijazo ambapo anatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Wakati huo huo mahakama kuu nchini Pakistan imemuidhinisha jenerali Pervez Musharraf kushiriki katika uchaguzi wa rais wa hapo kesho huku akiwa bado anashikilia madaraka ya kijeshi.

Hata hivyo lakini uamuzi huo wa mahakama kuu unamtia kitanzi jenerali Musharraf kwa kusema kwamba matokeo ya uchaguzi huo hayata tangazwa hadi tarehe 17 mwezi huu.

Mahakama mjini Islamabad inatarajiwa kutoa uamuzi juu ya pingamizi zilizowasilishwa iwapo rais Musharraf ana haki ya kutawala huku akiwa bado anashikilia madaraka ya kijeshi.

jenerali Musharraf alitangaza awali kuwa ataachia madaraka yake hayo ya kijeshi tarehe 15 mwezi Nov muda wake utakapo kamilika na kusubiri kuapishwa upya kama rais wa Pakistan wa kiraia.