ISLAMABAD : Musharraf atangaza hali ya hatari
3 Novemba 2007Matangazo
Wanajeshi na polisi wamezingira mahkama kuu mjini Islamabad ambayo inatarajiwa kutowa hukumu yake hivi karibuni juu ya uhalali wa ushindi wa Musharraf katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 6 Oktoba.
Kufuatia tangazo hilo matangazo ya vituo binafsi vya televisheni yamekatwa pamoja na mawasiliano yote ya simu.
Mshauri wa Musharraf amesema rais huyo atalihutubia taifa wakati wa usiku na kutowa ufafanuzi juu ya sababu za kutangaza hali hiyo ya hatari pamoja na katiba ya muda.