1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Jeshi lavamia msikiti na kuuwa 50

Wanajeshi wa Pakistan wameuvamia Msikiti Mwekundu leo hii katika mji mkuu wa Islamabad na kuuwa takriban wanamgambo 50 ambapo wanajeshi wanane pia wameuwawa.

Wanajeshi wamevamia eneo la msikiti huo kabla ya alfajiri na bado wamekuwa wakiendelea kujaribu kuwan’gowa wanamgambo waliojichimbia ndani ambao inasemekana kuwa wanawashikilia mateka watu 150.Watu wengi wamejeruhiwa katika shambulio hilo na wanamgambo 50 wametiwa mbarani.

Zadi ya theluthi mbili ya eneo hilo liko mikononi mwa wanajeshi.Msemaji wa kijeshi amesema sheik aliyeasi Abdul Rashid Ghazi amejichimbia katika vyumba vya chini vya msikiti huo akiwatumia wanawake na watoto kama ngao dhidi ya mashambulizi.

Wanamgambo wamekuwa wakijibu mashambulizi kwa kutumia maroketi,mabomu ya mkono na bunduki za rashasha.

Watoto kadhaa na akina mama wamefanikiwa kutoroka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com