1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran Yashtumu Marekani kwa sera za kucochea vita Iraq.

4 Mei 2007

Iran imezishutumu sera ya Marekani nchini Iraq,na kuilaumu nchi hiyo kwa vita vya kimadhehebu vilivyokithiri nchini Iraq. Matamshi hayo yametolewa na Waziri wa mambo ya nje wa Iran Manouchehr Mottaki katika mkutano wa Sharm El-Sheikh huko Misri. Mkutano huo umemalizika huku washiriki wakiafikiana kuimarisha vikosi vya kijeshi vya Iraq viweze kujisimamia wenyewe kuweka usalama.

https://p.dw.com/p/CHEp
Waziri wa mambo ya nje Condolezza Rice,katika mkutano wa Sharm El Sheik.
Waziri wa mambo ya nje Condolezza Rice,katika mkutano wa Sharm El Sheik.Picha: AP

Iran imezishutumu sera ya Marekani nchini Iraq,na kuilaumu nchi hiyo kwa vita vya kimadhehebu vilivyokithiri nchini Iraq. Matamshi hayo yametolewa na Waziri wa mambo ya nje wa Iran Manouchehr Mottaki katika mkutano wa Sharm El-Sheik huko Misri. Mkutano huo umemalizika huku washiriki wakiafikiana kuimarisha vikosi vya kijeshi vya Iraq viweze kujisimamia wenyewe kuweka usalama.

Ilitarajiwa kuwa Iran na Marekani wangekutana katika mkutano huo wa Sharm El -Sheik huko Misri, na yangekuwa mazungumzo ya kwanza katika miongo mitatu,lakini hilo halikotokea. Kwani waziri wa mambo ya nje wa Iraq Hoshiyar Zebari alisema ulikuwa tuu mkutano wa mabalozi na wajumbe wa Marekani na Iraq. Naye waziri wa mambo ya nje Codolezza Rice nikimnukuu alisema, "kungekuwa na nafasi ya kukutana na wairan,ningekutana nao lakini nafasi haikujitokeza’’

Waziri huyo wa Iran alisema licha ya kuwa hawakuweza kukutana na waziri Condolezza Rice,kukutana na wajumbe wengine wa Marekani ni dhihirisho kuwa maafahali hawa waili wanaweza kuafikiana katika siku zijazo.

Waziri huyo wa Iran alitaka wairani watano ambao wamezuiliwa na wanajeshi wa Marekani, Kaskazini mwa Iraq wawachiliwe, tetesi ambayo imeleta mzagarazano mkubwa baina ya mataifa hayo mawili kando na ile tetesi ya kinuklyea.

Waziri mkuu wa Iraq naye Nouri Maliki aliyataka mataifa jirani kukomesha ufadhili wa makundi ya kigaidi na kuwazuia kuingia nchini humo.

Mkutano huo ulimalizika kwa mataifa hayo kuahidi zaidi ya dolla billioni 15 ya misaada na baadhi yao kuahidi kufutilia mbali madeni ya Iraq,waliweka pia saini mkataba wa miaka mitano wa usaidizi wa kifedha. Lakini mkutano huo ulisistiza lazima serikali ya Iraq iimarishe demokrasia na maridhiano.

Waziri wa fedha wa Iraq Bayan Jabor alisema Misri imefutilia mbali mkopo wa dolla millioni mia nane huku Slovenia, Bulgaria na Poland wakifuta asilimia themanini ya mikopo yake.Umoja wa Ulaya na Uingereza wameahidi kutoa dolla millioni mia mbili.

Katika taarifa iliyotolewa kwa waandishi habari,washiriki wa mkutano huo wa Sharm El-Sheik kutoka mataifa ya Umoja wa ulaya,Mtaifa nane yalioyostawi kiviwanda pamoja na Syria na Iran,walisema wataunga mkono juhudi za kuimarisha vikosi vya Iraq ili viweze kuisimamia nchi yao wenyewe kiuslama.

Hatahivyo taarifa hiyo ilisema kuondoka kwa majeshi hayo Iraq kutategemea na mamuzi ya serikali yake. Mataifa mbalimbali ya kiarabu yametaka kutangazwa rasmi kwa siku ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini humo,jambo ambalo Waziri mkuu Nur Al Maliki wa Iraq na Marekani wamekataa kusema wazi.

Isabella Mwagodi.