Iran na Korea kaskazini yakumbwa na shinikizo la kuondoa mipango ya Kinuklya | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 30.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Iran na Korea kaskazini yakumbwa na shinikizo la kuondoa mipango ya Kinuklya

Mkutano wa mataifa wenye lengo la kuupa motisha utekelezaji wa mkataba wa kuzuwia utapakazaji wa silaha za kinuklya umetoa wito kwa serikali ya Iran na Korea kaskazini zikubali matakwa ya jumuiya ya kimataifa kuzitaka zipüunguze hofu iliopo kuhusu mipango yao ya kinyuklea.

Chini ya mkataba huu wa miaka 37 wa kuzuia kuenezwa silaha za kinuklyea,mataifa yasiyo na mipango ya kinuklya yameahidi kutosaka silaha hizo wakati mataifa yenye nguvu za kinuklyea duniani- Marekani,Urusi,Uingereza Ufaransa na China yakitakiwa kuturidhia kuzikongoa silaha zao za aina hiyo. Mataifa mengine matatu ambayo hayapo ndani ya mkataba huu ni Israel, India na Pakistan.

Utatuzi wa mzozo wa kinyukla wa Iran na makubaliano ya kukomesha kikamilifu mpango wa kinyukla wa korea kaskazini ikiwa yatafaulu, pia utachangia pakubwa katika kuzuia silaha za maangamizi duniani na kuafikia malengo ya kulifanya eneo la Mashariki ya kati kuwa bila silaha za maangamizi.

Na Umoja wa Ulaya umesema uko tayari kuhakikisha matumizi ya kinuklya Iran yamekomeshwa.Mjumbe Ruediger Luedeking anayeongoza ujumbe wa Ujerumani katika kikao hicho alisema Umoja wa Ulaya unataka baraza la Umoja wa Mataifa iwekee vikwazo Iran.

Mjumbe huyo wa Ujerumani pia ameitaka Korea kaskazini kuruhusu mataifa mengine kusimamia kuharibiwa kwa silaha zake za maangamizi pamoja na mizinga.

Kadhalika katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon alisisitiza mkataba huu wa kinyuklea wa NPT utiliwe maanani zaidi na mataifa haya. Ban Ki Moon aliutaja mzozobaina ya mataifa haya kama kitisho kikubwa kwa mkataba huo. Miaka miwili iliyopita mkutano wa mkataba wa NPT ulikumbwa na ugomvi dhidi ya ajenda yake ya kuzuia mataifa mengine kuwa na uwezo wa nguvu za kinyuklya.

Mkataba huo wa kuzuwia utapakazaji wa silaha za kinukleya- NPT- unasema kuwa mataifa tano yenye mipango ya kinyuklea kutoka wakati wa vita vya pili duniani,yaondoe silaha za maangamizi. Unaruhusu tuu mipango ya nishati ya nyuklea kwa ajili ya amani na maendeleo.

Lakini kutokana na jaribio la Korea kaskazini kulipua kombora la kinyuklya mwaka jana na uimarishaji wa mpango wa kinyukla wa Iran licha ya kuonywa na Umoja wa mataifa, umesababisha hali ya taharuki baina ya mataifa wanachama na kusababisha wao kutaka mikakati itakayozuia kuundwa kwa silaha za kinyuklea.

Mkatabu huu wa Kinuklyea NPT hupitiwa kila baada ya miaka mitano na mkutano mwengine wenye lengo hilo utafanyika 2010.

Isabella Mwagodi

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com