IRAN NA BARAZA LA USALAMA
24 Machi 2007Matangazo
UMOJA WA MATAIFA:
Baraza la Usalama la UM linatazamiwa hii leo kulipigia kura azimio la kuiwekea vikwazo zaidi Iran kutokana na mradi wake wa kinuklia.Azimio hilo litafuatia lile lililoidhinishwa na Baraza la Usalama desemba mwaka jana likidai kuwa Iran isimamishe mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium.
Rais Ahmadinejad amevunja safari yake aliopanga New York katika Umoja wa Mataifa ambako alitumai angeweza kuzungumza na Baraza la usalama kabla ya kura hiyo kupigwa. Amedai hakupata viza na mapema.