1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hotuba ya rais Obama mjini cairo ina lengo la kutafuta njia ya uhusiano mwema na mataifa ya Kiislamu.

Sekione Kitojo3 Juni 2009

Rais Barack Obama leo atatoa hotuba muhimu kwa mataifa ya Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu katika hatua ya kukaribiana na kuaminiana.

https://p.dw.com/p/I2xp
Rais Barack Obama alihutubia katika moja ya mikutano yake.Picha: AP

Hali ya wasi wasi baina ya nchi za Kiislamu na Marekani si mpya. Tangu kutokea shambulio la kigaidi la Septemba 11, hali inazidi kuwa ngumu. Uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Iraq na Afghanistan , hali ya kuendewa kinyume haki za binadamu katika gereza la Guantanamo na Abu Ghraib pamoja na hali ya wazi ya kutokuwa na nia kwa rais wa Marekani wa wakati huo George W. Bush kuhusiana na hatima ya Wapalestina imeongeza wasi wasi huo. Rais wa Marekani Barack Obama ana nia ya kuondoa hali hii. Ndio sababu leo Alhamis anatarajiwa kutoa hotuba muhimu mjini Cairo kwa mataifa ya Kiislamu.


Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush alijizuwia kila mara dhidi ya kutoa lawama, kuwa Marekani imo katika vita dhidi ya Uislamu. Tarehe 17 Septemba 2001 , siku sita baada ya shambulio la kigaidi mjini New York na Washington alisema, kuwa sura ya ugaidi sio sura halisi ya Uislamu, hii sio njia ya Uislamu, Uislamu ni amani. magaidi hawawakilishi amani bali uovu na vita.

Licha ya kuwa amekuwa akirudia maneno haya kila mara, katika ulimwengu wa Kiislamu hayakuwa yakiaminika. Kwa hiyo vita nchini Afghanistan na Iraq, pamoja na hali katika gereza la Guantanamo na Abu Ghraib lugha inakuwa nyingine kabisa.

Uvamizi nchini Iraq pamoja na mashambulio ya makombora kuelekea Pakistan ni vitu ambavyo katika siasa za Marekani vinasababu ya kuendeleza biashara yao ya silaha tu na sio kitu kingine.

Ujumbe huu wa George W. Bush mbali ya hayo haujaitoa Marekani katika mtazamo huo , anaelezea James Phillips kutoka wakfu wa kihafidhina wa Heritage, hasa kuhusiana na hotuba ya Obama mjini Cairo.

Katika nyakati fulani ni muendelezo wa sera za Bush, lakini kwa mtazamo mwingine, na ni matumaini kuwa tuna nafasi kubwa ya kupeleka ujumbe katika ulimwengu wa Kiislamu.


Kwa kweli hata katika utawala wa rais Obama mashambulio ya makombora ya Marekani dhidi ya maeneo ya Pakistan yanaendelea. Ni kweli kwamba Obama anafuata siasa za kusikiliza zaidi.

Anataka kuielekea Iran. Uamuzi wa kulifunga gereza la Guantanamo umekwisha fikiwa, hata kama hatua ya utekelezaji ni ngumu. Kwa kweli matamshi ya Obama yanatofauti kubwa hata hivyo na yale ya mtangulizi wake. Wakati wa hotuba yake alipoingia madarakani Januari mwaka huu alisema , kuwa Marekani haimo na kamwe haitakuwamo katika vita na Uislamu.

Mahojiano yake ya kwanza katika televisheni baada ya uchaguzi yalikuwa na kituo cha televisheni cha Uarabuni, katika ziara yake ya kwanza katika bara la Ulaya alieleza mjini Ankara , kuwa Marekani haiko katika vita dhidi ya Uislamu na hali hiyo haijabadilika.

Hotuba ya rais Obama mjini Cairo inapaswa kutilia maanani mantiki ya sera hii , anasema mwakilishi wa mshauri wa masuala ya usalama , Dennis McDonough, katika mazungumzo ya simu. Rais Anafahamu kuwa mafanikio ya dunia yetu hii ya kisasa yametokana na utafiti uliofanyika katika ulimwengu wa Kiislamu na mtu anahitaji kurejea katika uhusiano ambao ulikuwapo karne kadha zilizopita. Tunafahamu pia kuwa Cairo pamechaguliwa kwa tukio hili kutokana na umuhimu wa vyuo vyake vikuu.

►◄



Mwandishi: Bergmann , Christina

Imetafsiriwa na Sekione Kitojo.