Himid: Hata nikivuliwa uwanachama wa CCM, sitabadili mawazo yangu kuhusu Muungano | Matukio ya Afrika | DW | 25.07.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Himid: Hata nikivuliwa uwanachama wa CCM, sitabadili mawazo yangu kuhusu Muungano

Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, Mansour Yusuf Himidi, amesema atasimamia mtazamo wake kuhusu muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaofaa hata kama itapelekea kuvuliwa uwanachama.

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume.

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume.

Mwandishi wa DW Zanzibar, Salma Said, amefanya mahojiano na Mansour Yusuf Himidi, ambaye ni waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusiana na kauli za Katibu Mwenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, na wajumbe wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, kumtaka arudishe kadi ikiwa hakubaliani na sera ya sasa ya serikali mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kusikiliza mahojiano hayo, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mahojiano: Salma Said/Mansour Y. Himidi
Mhariri: Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada