1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Hillary Clinton awasifu waasi wa Libya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, amewasifu waasi wa Libya kwa kufanikiwa kumng’oa madarakani Kanali Muammar Gaddafi.

default

Hillary Rodham Clinton

Mwanadiplomasia huyo alito ahadi kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kulisaida baraza la mpito la waasi wa Libya kurejea katika mkondo wa demokrasia.

Akizungumza na viongozi wa Baraza hilo mjini Tripoli; Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alisema kuwa Walibya waliupiga vita udikteta uliokuwako na wamefanikiwa kurejesha haki za taifa lililo huru.

Flash-Galerie Kämpfe um Sirte Libyen

Mapambano makali yaendelea Sirte: ngome ya mwisho ya Kanali Gaddafi iliyosalia.

Bibi Clinton alisisitiza kuwa Marekani itauunga mkono mfumo utakaoyapa kipa umbele masuala ya demokrasia na makundi yanayotaka kuivuruga mipango hiyo yatalazimika kupambana na Walibya wenywewe.

Libyen Machthaber Gaddafi TV Auftritt Vertreter Stämme

Kanali Moammar Gadhafi, bado hajulikani aliko.

Hillary Clinton aliwasili kwenye mji mkuu wa Libya wa Tripoli, akiwa katika ziara ambayo haikutarajiwa. Wakati huohuo mapambano makali yanaripotiwa kuendelea mjini Sirte alikozaliwa Kanali Gaddafi. Sirte ni ngome yake ya mwisho muhimu iliyosalia.

Mwandishi: Mwadzaya,Thelma-ZPR

 • Tarehe 19.10.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/12uyp
 • Tarehe 19.10.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/12uyp

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com