1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wahudhuria mazishi ya Helmut Schmidt

23 Novemba 2015

Macho ya wajerumani yanakodolewa Hamburg ambako kansela wa zamani wa kutokaa chama cha SPD Helmut Schmidt aliyefariki dunia Novemba 10 akiwa na umri wa miaka 96,anaagwa rasmi na kwa heshima zote mjini Hamburg.

https://p.dw.com/p/1HAZj
Deutschland Staatsakt für Helmut Schmidt in Hamburg - Angela Merkel
Picha: Reuters/T. Schwarz

Takriban wiki mbili baada ya Helmut Schmidt kuiaga dunia,viongozi mashuhuri kutoka nyanja za kisiasa,wageni kadhaa kutoka nje na ndani na wajerumani kwa jumla,wanamwaga kansela huyo wa zamani wa Ujerumani.Buriani hizo rasmi zilizoandaliwa na rais wa shirikisho Joachim Gauck zinafanyika wakati huu tulio nao katika kanisa kuu la St.Michaelis au-dem "Michel" huku hatua za ulinzi zikiimarishwa katika eneo hilo .Mbali na rais wa shirikisho Joachim Gauck, na kansela Angela Merkel,buriano hizo zinahudhuriwa pia na wawakilishi wa ngazi ya juu wa taasisi muhimu za Ujerumani;spika wa bunge la shirikisho Bundestag Norbert Lummert,spika wa baraza la wawakilishi wa majimbo Stanislaw Tillich na mwenyekiti wa korti ya katiba Andreas Voßkuhle.

Nje ya Ujerumani buriani hizo rasmi zitahudhuriwa miongoni mwa wengineo na rafiki mkubwa na wa muda mrefu wa Helmut Schmidt,rais wa zamani wa Ufaransa Valérie Giscard d'Esteing,waziri mkuu wa zamani wa Itally Giorgio Napolitano na katibu mkuu wa jumuia ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg.Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker na spika wa bunge la Ulaya Martin Schulz pia watahudhuria buriani hizo.

Deutschland Staatsakt für Helmut Schmidt in Hamburg - Valéry Giscard d’Estaing
Rafiki mkubwa wa marehemu Schmidt,rais wa Zamani wa Ufaransa Valérie Giscard d'EsteingPicha: Getty Images/S. Gallup

Hishma zote za kijeshi kumuaga Helmut Schmidt

Mwishoni mwa maombolezi,hotuba na sifa,mwanasiasa huyo wa chama cha SPD ataagwa kwa hishma zote za kijeshi,kabla ya wanajeshi kulibeba jeneza lake kutoka kanisa la Saint Michaelis au dem Michel kama linavyojulikana,na kuzunguka foleni ya kikosi cha heshima cha jeshi la shirikisho Bundeswehr kabla ya kutiwa ndani ya gari na kusindikizwa na kikosi cha heshima cha polisi kuelekea ofisi ya meya na baadae kusafirishwa kilomita 12 hadi katika kiunga cha makaburi cha Ohlsdorf.Huko ndiko mwili wa Helmut Schmidt utakakochomwa moto na jivu kuzikwa ndani ya kaburi la familia.

Kiongozi mstahiki mwenye maadili

Helmut Schmidt amefariki dunia kiwa na umri wa miaka 96, novemba kumi iliyopita akiwa nyumbani kwake mjini Hamburg.Mwanasiasa huyo wa chama cha Social Democratic ameiongoza Ujerumani kuanzia mwaka 1974 hadi 1982.Katika enzi zake mtaalam huyo wa kiuchumi alikabiliana na mizozo kuanzia ule wa mafuta hadi kufikia mapambano dhidi ya magaidi wa Roten Armee Fraktion au kundi la jeshi jekundu".Hata mabishano kuhusu kile kilichokuwa kikijulikana kama uamuzi wa ncha mbili wa jumuia ya kujihami ya NATO yaligubika utawala wake.Hata kama kulikuwa na waliokuwa wakiutia ila uongozi wake, utuuzimani mwake,Helmut Schmidt ambae pia anamiliki shirika la kuchapisha vitabu na mwasisi wa jarida la "Die "Zeit" amejipatia sifa za kuwa kiongoziwa mstahiki wa Ujerumani mwenye kupigania maadili.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/epd/dpa

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman