HEILEGENDAMM: Waandamanaji wajumuika karibu na mkutano wa G8 | Habari za Ulimwengu | DW | 02.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HEILEGENDAMM: Waandamanaji wajumuika karibu na mkutano wa G8

Siku chache tu kabla ya kuanza mkutano wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8, katika mji wa kitalii wa Heilegendamm, watu kiasi laki moja wanaopinga utandawazi wamejumuika tayari kuandamana katika mji Rostock karibu na mahali pa mkutano.

Waandamanaji hao wanaandamana kupinga sera za mataifa hayo manane.

Kiasi polisi elfu kumi na tatu wamepelekwa katika mji huo ili wazuie ghasia.

Jana mahakama moja ya Ujerumani ilitoa uamuzi wa kuwazuia waandamanaji kuukaribia mji wa Heilegendamm wakati wa mkutano huo utakaonza tarehe sita na kumalizika tarehe nane mwezi huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com