1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA: Fidel Castro bado anaula !

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyI

Televisheni ya Cuba imemwonyesha aliekuwa kiongozi wa nchi hiyo Fidel Castro akitembea na kusema kuwa watu wametabiri kifo chake mapema mno.! Kiongozi huyo wa Cuba ambae sasa ana umri wa miaka 8o hajaonekana hadharani tokea mwezi wa septemba baada ya kulazwa hospitalini.

Katika ukanda wa video uliooneshwa na televisheni Fidel Castro ameonekana akisoma gazeti la kikomunisti Granma.

Hivi karibuni kulikuwa na uvumi mkali kwamba kingozi huyo ameshafariki.