1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harare. Tsvangirai apigwa na polisi hadi kuzirai.

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJe

Wanachama wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe , Movement for Democratic Change wamesema kuwa kiongozi wao amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na polisi.

Wamesema kuwa Morgan Tsvangirai , ambaye anashikiliwa na polisi , alizirai mara tatu baada ya kupigwa, na huenda hali yake ni mbaya sana.

Mawakili wanaomtetea wametoa hati mahakamani ili kuwaruhusu kupata mawasiliano nae pamoja na kumpatia msaada wa hospitali. Alikuwa mmoja kati ya viongozi kadha wa upinzani ambao walikamatwa wakati polisi wa kuzuwia ghasia walipovunja mkutano sala ambayo ilikuwa ikifanyika dhidi ya serikali siku ya Jumapili.

Muungano wa vyama vya upinzani , kanisa na makundi ya kijamii yaliitisha mkutano huo kujadili mzozo wa kisiasa na kiuchumi nchini Zimbabwe.

Wanamlaumu Robert Mugabe kwa uhaba wa chakula pamoja na ughali wa maisha ambao unafikia kiasi cha asilimia 1,600.