HANOI: Uhusiano wa kibalozi kuanzishwa kati ya Vietnam na Vatikan | Habari za Ulimwengu | DW | 01.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HANOI: Uhusiano wa kibalozi kuanzishwa kati ya Vietnam na Vatikan

Rais Generali Pervez Musharraf wa Pakistan.

Rais Generali Pervez Musharraf wa Pakistan.

Vietnam na Vatikan zinataka kuanzisha uhusiano wa kibalozi.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya kikomunisti mjini Hanoi,mada hiyo ilijadiliwa wakati wa ziara ya waziri mkuu Nguyen Tan Dung hapo Januari 25,ambapo alikutana na Papa Benedikt wa XVI.Lakini hakusema uhusiano huo wa kibalozi utaanzishwa lini.Katika bara la Asia,baada ya Ufilipino,Vietnam ni nchi yenye idadi kubwa sana ya Wakatoliki,ikiwa ni asilimia 10 ya umma wa Vietnam wa milioni 84.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com