1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANNOVER:Kansela Schroeder hatokuwepo katika serikali mpya ya Ujerumani

13 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESX

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amethibitisha kuwa hatokuwemo katika serikali mpya itakayoongozwa na Angela Merkel wa chama cha kihafidhina cha CDU.Lakini atashiriki katika majadiliano ya kuundwa serikali ya muungano yatakayofanywa kati ya chama chake cha SPD na vyama vya kihafidhina vya CDU na CSU.Schroeder, alitoa taarifa hiyo siku ya Jumatano kwenye mkutano wa vyama vya wafanyakazi mjini Hannover.Schroeder alieiongoza Ujerumani tangu mwaka 1998,alikubali kuondoka madarakani,baada ya kupata makubaliano kuwa chama chake cha Social Democrats kitapewa sehemu kubwa ya nyadhifa 14 za wizara,ikiwa ni pamoja na wizara ya mambo ya kigeni na ya sheria.Chama cha CDU kitakuwa na nyadhifa 6,zikiwemo za uchumi,mambo ya ndani,ulinzi pamoja na spika wa bunge.Siku ya Jumatatu,chama cha CDU cha Bibi Merkel na SPD cha Kansela Schroeder,vilitangaza kuwa vimekubali kimsingi kuunda kile kinachoitwa serikali ya Muungano Mkuu.