1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali yakutisha yarejea Bangkok

19 Mei 2010

Hali katika mji mkuu wa Thailand Bangkok inaelekea kurejea kuwa tete, baada ya askari pamoja na magari ya kijeshi wakilizingira eneo la kibiashara ambalo linadhibitiwa na maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali

https://p.dw.com/p/NRRB
Waandamanji wa mashati mekundu wakiwa tayari kupambana na polisi mjini BangkokPicha: AP

Kiongozi mmoja wa waandamanaji hao Nattawut Saikua amesema wanajiandaa kukabiliana harakati hizo za serikali.Milio ya risasi imeendelea kusikika kutoka katika eneo hilo.Hapo jana serikali ya Thailand ilikataa upatanishi uliyotangazwa na Baraza la Seneti la nchi hiyo.

Afisa mmoja wa serikali hiyo alisema kuwa serikali itakuwa tayari kwa mazungumzo iwapo waandamanaji hao wataondoka kutoka katika eneo hilo.

Kiasi ya watu 39 wamekwishauawa mpaka sasa tokea kuibuka kwa mapigano mitaani kati ya polisi na waandamanaji hao Alhamisi iliyopita.

Mwandishi:Aboubakary Liongo