1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya kisiasa visiwani Zanzibar

21 Januari 2010

Balozi wa Tanzania Italy, Ali Karume, ambaye amekwishatangaza nia yake ya kutaka kuwania kiti cha urais Zanzibar, ameibuka na kupinga vikali hoja ya kutaka Rais Amani Karume, aongezewe muda wa miaka miwili.

https://p.dw.com/p/LdAo

Katika mahojiano yake na Aboubakary Liongo, Balozi Karume amesema muafaka uliofikiwa kati ya Rais Karume na Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ni suala ambalo alilipigia kelele hadharani lifanyike miaka miwili iliyopita na kujinasibu kuwa yeye ni sheikh Yahya Hussein wa siasa, akimaanisha yule mtabiri wa masuala ya siasa.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Othman Miradji