Hali ya Kisiasa visiwani Zanzibar
26 Novemba 2009Matangazo
Visiwani Zanzibar, siku chache baada ya Rais Karume na Chama kikuu cha upinzani visiwani humo CUF kutangaza hadharani kuzika tofauti zao na kuashiria kuwepo kwa serikali ya mseto, baadhi ya wanasiasa vigogo wa chama tawala CCM visiwani wamejitokeza kulipinga wazo hilo, katika kile wengine wanachokiona kuwa kama ni kupingana na mtazamo wa rais Karume
Hata hivyo wananchi wazipokea kauli za wanasiasa kwa hisia tofauti, kama anavyoarifu zaidi mwandishi wetu wa Zanzibar Salma Said
Mpitiaji:Aboubakary Liongo
Mhariri:Abdul-Rahman