1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya kisiasa nchini Kenya

22 Februari 2008

Nchini Kenya leo ni siku ambapo tangazo la waziri mkuu mpya linasubiriwa kufuatia muafaka wa hapo jana wa kuunda wadhifa huo mpya.

https://p.dw.com/p/DBsJ
Raila Odinga kiongozi wa ODM safarini NigeriaPicha: AP Photo
Mazungumzo ya kutafuta amani yanayoendelea kwa yapata majuma mawili yameingia hatua nyeti chini ya uongozi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wa zamani Koffi Annan. Wakati huo huo kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement ODM Bw.Raila Odinga anaripotiwa kuondoka nchini kwa ndege binafsi na kutarajiwa kurudi hapo kesho. Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja katika uwanja wa ndege, Bw.Odinga ameelekea nchini Nigeria. Ili kupata thibitisho kuhusu taarifa hizo Thelma Mwadzaya alizungumza na William Ruto mmoja wa viongozi wa chama cha ODM aliye pia mbunge wa Eldoret Kaskazini.