Hali tete yajitokeza Komoro kufuatia kuuwawa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais
14 Juni 2010Matangazo
Mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais Ahmed Abdullah Sambi katika visiwa vya Comoro Kanali Kombo Ayuba amepigwa risasi na kuuwawa. Kanali huyo alipigwa mlolongo wa risasi wakati akishuka garini nyumbani kwake katika mji mkuu Moroni.
Aboubakar Liongo alizungumza kwa njia ya simu na mchambuzi na mhadhiri katika chuo kikuu cha Comoro, Profesa Ibrahim Mohamed Ibrahim ambaye kwanza alinieleza juu ya hali ilivyo wakati huu baada ya tukio hilo.
Mahojiano:Liongo/Prof Ibrahim Mohamed
Mpitiaji:Abdul-Rahman