Hali sasa ni tulivu nchini Guinea | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.09.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hali sasa ni tulivu nchini Guinea

Hali ya utulivu imerejea tena katika mji mkuu wa Guinea -Conakry ingawa bado ni tete.

default

Kapteni Moussa Dadis Camara wa Guinea

Viongozi wa upinzani wamekula kiapo kuendelea na maandamano ya kuupinga utawala wa kijeshi wa Kapteni Moussa Dadis  Camara, baada ya watu 157 kuuawa pale  wanajeshi walipofyatua risasi dhidi ya  waandamanaji Jumatatu iliopita. Maandamano hayo yaliitishwa na wanasiasa  wa upinzani kupinga mpango wa  Kiongozi wa kijeshi kutaka kuwa mgombea  katika uchaguzi ujao  akiwa na lengo la kubakia madarakani, licha ya kusema wakati alipotwaa madaraka kuwa  hakuwa na azma hiyo. Mohamed AbdulRahman amezungumza  na  Mwandishi Habari na mchambuzi wa masuala ya Afrika Jenerali Ulimwengu  akiwa Dar es salaam, na kwanza alimuuliza  matukio haya yanaashiria nini katika siasa za Guinea chini ya uongozi wa sasa .

Mtayarishaji: Mohamed Abdulrahman

Mhariri: Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

 • Tarehe 30.09.2009
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Juxf
 • Tarehe 30.09.2009
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Juxf

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com