Hali ni shwari Uingereza baada ya polisi kumwagwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.08.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hali ni shwari Uingereza baada ya polisi kumwagwa

Kuwapo na polisi wengi zaidi katika miji mikubwa ya Uingereza hadi sasa kumezuwia ghasia , kukiwa hakuna ripoti za ghasia usiku wa jana.

default

Majirani wakijaribu kusafisha mji baada ya ghasia za uchomaji magari na majengo katika eneo la Clapham mjini London

Kuwapo na polisi wengi zaidi katika miji mikubwa ya Uingereza hadi sasa kumezuwia usiku wa tano wa ghasia, kukiwa hakuna ripoti za ghasia kubwa. Mapema jana , waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ameahidi kumaliza kile alichokiita ghasia za kuchukiza nchini humo. Amesema kuwa iwapo ghasia zitaendelea, polisi huenda wakaamua kutumia silaha ya mabomba ya maji kwa mara ya kwanza nchini Uingereza. Maafisa 16,000 wa polisi wamewekwa katika mji wa London kwa usiku wa pili hii leo. Miji mingine kaskazini na kati ya Uingereza kama Manchester, Liverpool na Birmingham, ambayo imeshuhudia ghasia mbaya zaidi siku ya Jumanne usiku, pia inaonekana kuwa shwari. Zaidi ya watu 1,000 wamekamatwa, ambapo watu 805 wamekamatwa mjini London pekee. Katika ishara ya kuchukua hatua za haraka za kisheria, maafisa mjini Manchester wametoa hukumu na watu wawili wamehukumiwa kifungo.

 • Tarehe 11.08.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/12Epz
 • Tarehe 11.08.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/12Epz

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com