Hali ni shwari katika visiwa vya Komoro
15 Juni 2010Matangazo
Kombo Ayouba alipigwa risasi na mtu au watu wasiojulikana wakati alipowasili nyumbani kwake Jumapili usiku. Matukio haya yanajiri katika wakati ambao uchaguzi wa rais umepangwa Novemba mwaka huu, na ni zamu ya kisiwa cha Mwali kuchukuwa wadhifa huo ambapo kitawasilisha wagombea watakaopigiwa kura na visiwa vyote vitatu.
Nimezungumza na Spika wa zamani wa bunge la Comoro, Mohamed said Mshangama, na kwanza nilimuuliza hadi sasa ni kipi kilichofahamika kuhusiana na kuuawawa kwa Kanali Kombo Ayouba.
Mahojiano :Mohamed Abdul-Rahman/Mohamed Said Mshangama.
Mpitaiaji:Miraji Othman