1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali nchini Somalia

14 Februari 2007

Nchini Somalia hali inaelekea kuwa mbaya ambapo wapiganaji wa mahakama za kiislamu waliyofurushwa na majeshi ya Ethiopia wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

https://p.dw.com/p/CHKG
Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia Ali Mohamed Gedi
Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia Ali Mohamed GediPicha: AP

Kumeripotiwa mashambulizi ya maguruneti katika nyumba ya waziri wa biashara wa Somalia mjini Mogadishu na mengine yakafanyika katika bandari ya Somalia. Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia Ali Mohamed Gedi amelaani mashambulizi hayo na kutaka kufikishwa mbele ya sheria kwa wanamgambo hao wa kihafidhina. Hali hiyo inakuja huku juhudi zikifanyika za kupelekwa haraka kwa kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani nchini Somalia.

Muda mfupi uliopita maafisa wa umoja huo walimaliza kikao chao mjini Addis Ababa juu ya mzozo huo, Abubakar Liongo aliwasiliana na mwakilishi wa Umoja huo katika mzozo wa Somalia, Balozi Mohamed Foum.