1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ingali tete Somalia

Maurus,Hans-Jürgen/ZPR20 Januari 2012

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hali ingali mbaya nchini Somalia. Kiasi ya watu milioni nne wanahitaji msaada wa dharura ama sivyo kutatokea maafa makubwa ya kibinadamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/13n1a
A worker from Kuwait Red Crescent carries a sack of rice after a ship carrying a consignment of food for refugees docked at Mogadishu seaport, Somalia Sunday July 31, 2011. Tens of thousands of famine-stricken Somali refugees were cold and drenched after torrential rains overnight pounded their makeshift structures in the capital, Mogadishu. Rains are needed to plant crops and alleviate the drought that is causing famine in Somalia but on Saturday night the rains added to the misery of refugees who live in structures made of sticks and pieces of cloth. (Foto:Mohamed Sheikh Nor/AP/dapd)
Msaada wa dharura wahitajiwa kuzuia maafa ya kibinadamu SomaliaPicha: dapd

Mzozo wa Somalia haujamalizika kwani licha ya maendeleo madogo kupatikana mwaka uliopita, maisha ya watu 250,000 yangali hatarini. Hayo amesema, mratibu wa misaada ya kiutu ya Umoja wa Mataifa kwa Somalia, Mark Bowden. Akiomba msaada wa dola bilioni 1.5 kutoka kwa wafadhili wa kimataifa alisema:

"Hali bado ni tete nchini Somalia. Hadi watu milioni nne wanahitaji msaada wa aina moja au mwingine."

Sasa Umoja wa Mataifa ndio umetoa wito mpya kuomba msaada wa dharura ili kuzuia maafa zaidi. Umasikini mkubwa, mavuno mabaya na idadi kubwa ya mifugo inayokufa ni miongoni mwa mambo yanayozidisha matatizo ya watu hao katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Bei ya vyakula pia imeongezeka kwa asilimia 200 katika miaka iliyopita. Lakini vile vile kuna maendeleo kadhaa anasema, mratibu huyo wa misaada ya kiutu.

Kwa mfano, katika wilaya tatu, tatizo la njaa halipo tena. Watu wapatao milioni 2.6 wamepatiwa chakula: watu milioni 1.2 wanapata maji safi. Watoto milioni 1 wamechanjwa dhidi ya surua. Hiyo ni asilimia 51 ya umma uliolengwa kuchanjwa.
Hata hivyo, bado kuna matatizo makubwa anasema, Mark Bowden. Kwa maoni yake, ni lazima kuhakikisha usalama wa chakula. Mzozo wa chakula utaanza kupungua pale mavuno ya pili ya Somalia yatakapopatikana yaani katika miezi ya Agosti na Septemba. Tatizo jingine kuu ni hali ya wakimbizi anaeleza mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa, Mark Bowden.

"Mji mkuu Mogadishu unashughulikia wakimbizi wapya. Watu hao wapatao kama 185,000 wanategema misaada kutoka nje ili kuweza kuishi."


Lakini mashambulio yanayowalenga wafanyakazi wa mashirika ya misaada ni tatizo kubwa pia. Shirika la "Madktari wasio na mipaka" linaondoka kutoka maeneo ya mapigano mjini Mogadishu baada ya wafanyakazi wake wawili kuuawa. Hata chama cha kimataifa cha msalaba mwekundu kimesita kusafirisha chakula kusini mwa Somalia baada ya malori 140 kuzuiliwa na maafisa wa eneo hilo la kusini. Vile vile katika majuma ya hivi karibuni, mashambulio ya anga kutoka Kenya yameshika kasi katika eneo la Chuba kusini mwa Somalia.

epa02950038 A burning car is seen at the scene of a car bomb explosion in war-torn Somalia's capital Mogadishu, 04 October 2011. Reports state that more than 50 people have been killed after a vehicle exploded in front of the Ministry of Education building. Al Qaeda-linked Islamic militia al-Shabab has claimed responsibility for the deadly attack. EPA/ABDI HAJJI HUSSEIN
Mashambulio yanahatarisha kazi za mashirika ya misaadaPicha: picture-alliance/dpa