1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Hali inasemekana ni shuwari katika jamahuri ya kidemokrasi ya Kongo

Kinshasa

Hali ni shuwari katika mjamhuri ya kidemokrasi ya Kongo,siku moja baada ya kutangazwa Joseph Kabila mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini humo kwa asili mia 58.05.Macho ya wakongomani na walimwengu kwa jumla yamekodolewa katika kambi ya Umoja kwaajili ya taifa,UN ya makamo wa rais wa zamani Jean Pierre Bemba amejikingia takriban asili mia 42.Naibu mkurugenzi wa kambi ya Umoja kwaajili ya taifa Fidèle Babala amesema watatangaza msimamo wao baadae hii leo au kesho.Bwana Babala ambae pia ni mkurugenzi wa ofisi ya makamo wa rais amehakikisha kambi ya Bemba haichochei fujo na itajiandaa kuwajibika kama chama cha upinzani bungeni.Wakati huo huo kambi ya rais mteule Joseph Kabisa imetoa mwito wa kuwepo umoja na suluhu nchini.Msemaji wa kambi ya AMP -Muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais Olivier Kamitatu aliahidi kila mkongomani atapata nafasi anayostahiki na uhuru wa kutoa maoni yake kwa masilahi ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.Matokeo ya uchaguzi yanabidi yaidhinishwe na korti kuu nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com