1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna ratiba ya kuwahamisha wanajeshi wa Uengereza anasema waziri wa mambo ya nchi za nje Margaret Beckett

28 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyL

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uengereza Margaret Beckett ameionya serikali ya Irak isihatarishe umoja wa taifa kwasababu ya masilahi ya kisiasa.Akizungumza na jarida la Ujerumani Der Spiegel,waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Uengereza Margaret Beckett amesema wanasiasa waliochaguliwa wasiigawe nchi kwa sababu ya masilahi yao.Badala yake wanabidi wajitahidi kuimarisha amani na usalama.Waaziri huyo wa Uengereza amesisitiza hakuna ratiba maalum iliyopangwa kuwahamisha wanajeshi elfu sabaa wa uengereza toka Iraq.