1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres aipigia chapuo nishati jadidifu Afrika

Iddi Ssessanga
5 Septemba 2023

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres ameihimiza jumuiya ya kimataifa kusaidia kuifanya Afrika kuwa nguvu ya nishati jadidifu wakati wa mkutano wa kilele wa tabianchi unaolenga kuvutia uwekezaji wa kimazingira Afrika.

https://p.dw.com/p/4VyX8
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GutteresPicha: Xie E/XinHua/dpa/picture alliance

Mkutano huo wa siku tatu wa kilele ulioanza jsiku ya Jumatatu, umewashirikisha wakuu wa nchi, serikali na viwanda, wakiwemo viongozi kutoka Msumbiji na Tanzania, pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na mjumbe maalumu wa serikali ya Marekani anaeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi John Kerry.

Akizungumza kwenye Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutgerres amesema nishati jadidifu inaweza kuwa muujiza wa Afrika, lakini akaongeza kuwa sisi ndiyo tunapaswa kulifanya hilo litokee.

Huku dunia ikiwa imepungukiwa kana katika utekelezaji wa malengo yake ya kupunguza ongezeko la joto, Guterres amezungumza moja kwa moja na viongozi wa kundi la mataifa 20 yaliostawi na ya yanayoinukia kiuchumi duniani, G20, wanaokutana nchini India mwishoni mwa juma hili, na kuwataka kuchukuwa majukumu yao katika mapambano ya kupunguza joto la dunia.

"Leo nimerudia wito wangu kwa ulimwengu kuharakisha hatua za hali ya hewa ili kuepusha athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi, kutimiza ahadi za kimataifa za kutoa msaada muhimu na kusaidia Afrika kufanya mabadiliko ya haki na ya usawa kwa nishati mbadala," alisema Katibu Mkuu Guterres.

Nairobi Kenya | mkutano wa ACS23 | William Ruto, Rais wa Kenya
Rais wa Kenya na mwenyeji wa mkutano wa ACS23, William Ruto.Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

UAE kuwekeza dola bilioni 4.5 miradi ya mazingira

Nishati safi ya mpito katika mataifa yanayoendelea duniani itakuwa muhimu ili kuweka hai lengo la Makubaliano ya Paris la kupunguza ongezeko la joto duniani  chini ya kiwango cha nyuzi joto mbili cha wakati wa kabla ya viwanda, na 1.5C ikiwezekana.

Ili kufanikisha hilo, Shirika la Nishati la Kimataifa linasema uwekezaji utahitaji kuongezeka hadi dola 2 trilioni kwa mwaka ndani ya muongo mmoja, hili likiwa ongezeko la mara nane.

Soma pia: Viongozi wa Afrika wakutana kujadili mazingira Nairobi

Hii leo mkutano huo umeshuhudia ahadi yake muhimu zaidi kufikia sasa, ambapo Umoja wa Falme za kiarabu umetowa dola bilioni 4.5 za kupambana na uchafuzi wa mazingira. Umoja wa Falme za Kiarabu UAE,  pia utakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa COP28 mjini Dubai mwezi Novemba hadi Desemba.

Sultan Al Jaber, ambaye anaongoza kampuni ya kitaifa ya mafuta ya UAE ADNOC na kampuni ya nishati mbadala inayomilikiwa na serikali ya Masdar, amesema uwekezaji huo utaanzisha miradi kadhaa muhimu ya nishati safi barani Afrika.

"Mpango huu umeundwa kufanya kazi na Afrika na kwa ajili ya Afrika. Utakuwa kama kielelezo kizito ambacho kinaweza na kinafaa kuigwa, na kitaunga mkono lengo la kimataifa la COP 28 la kuongeza mara tatu nishati jadidifu ifikapo 2030," alisema Al Jabir, amabye ni mwenyekiti wa mkutano ujao wa COP28 mjini Dubai.

Kenia Nairobi |Mkutano wa kilele wa mazingira Afrika 2023 | Wajumbe
Wajumbe wanaoshiriki mkutano wa ACS wakiwa katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Kenyatta, KICC mjini NAirobi, Kenya, Septemba 4, 2023.Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

EU kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi Afrika

Kwa upande wake rais wa halmashauri kuu ya umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesisitiza ahadi ya Umoja wa Ulaya kuisaidia Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kutoa kile alichowasilisha kama fursa za manufaa kwa mabara yote mawili.

Akizungumza katika mkutano huo, Von der Leyen ametilia mkazo umuhmu wa uwekezaji wa kifedha barani Afrika, ili kukuza niashati rafiki kwa mazingira.

Hata hivyo msisitizo wa mkutano huo kuhusu baadhi ya mapendekezo ya ufadhili wa hali ya hewa umeibua upinzani kutoka kwa baadhi ya watetezi wa mazingira, huku mamia ya waandamanaji wakiandamana karibu na ukumbi wa mkutano jijini Nairobi siku ya ufunguzi.

Chanzo: Mashirika