1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA:Ethiopia na Eritrea kupunguziwa majeshi ya usalama

17 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCa2

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linaunga mkono pendekezo la kupunguza kikosi cha Umoja huo cha kulinda amani nchini Ethiopia na Eritrea kutoka wanajeshi alfu 2300 hadi alfu 1700.Kulingana na Baraza hilo idadi hiyo bado itaweza kusimamia shughuli za kulinda usalama katika eneo hilo la mpakani linalozua mvutano mkali kati ya mataifa hayo mawili ya eneo la Pembe ya Afrika.Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin aliye mwenyekiti wa baraza hilo kwa sasa anasema kuwa baadhi ya wanachama wanavunjwa moyo na kusuasua kwa shughuli ya kuweka mpaka katika eneo hilo linalozozaniwa.

Baraza hilo la Usalama linatathmini ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa wa zamani Koffi Annan iliyoeleza kuwa mzozo huo unasababishwa na kusuasua kwa shughuli hiyo ya kuweka mpaka kati ya nchi za Ethiopia na Eritrea.Kikosi kilicho na majeshi alfu 2300 kimekuwa kikishika doria katika eneo hilo la mpakani lililo na urefu wa kilomita alfu moja chini ya makubaliano yaliyofikiwa mwisho wa mwaka 2000.Maafikiano hayo yalimaliza vita vilivyodumu miaka miwili u nusu katika eneo hilo la mpakani.