1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gazetini-Steinmeier na timu yake.

30 Julai 2009

Usuhuba mpya kati ya Marekani na China.

https://p.dw.com/p/J08M
Schumacher arejea Ferrari.Picha: AP

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumanii hii leo, yamegusia mada mbali mbali tangu za ndani hata nje ya nchi:

Nje ya Ujerumani ,wahariri wameuchambua usuhuba mpya katii ya Marekani na China.Ndani,wameichambua timu mpya ya mtetezi wa wadhifa wa ukanzela wa Ujerumani kwa tiketi ya chama cha SPD -waziri wa nje Frank Steinmeier kwa jicho la kashfa ya waziri wa afya kutokla chama chake bibi Ulla Schmidt.

Gazeti la Emder Zeitung juu ya usuhuba kati ya Marekani na China,laandika:

"Wamarekani na machina wamekutana huko Washinghton kwa kikao muhimu cha uchumi na cha kutunga mkakatzi wa pamoja.Mwishoe ,matokeo yake yalikuwa wazi-nayo ni kwamba pande zopte mbili zinataka kushirikiana kwa nguvu zaidi katika nyanja zote za kisiasa.Lakini, matokeo ya mkutano wao kama huo,yasiwekewa matumaini makubwa.Kwani, karatasi ina uvumilivu mkubwa.

Muhimu zaidi kuliko maafikiano hayo yaliofikiwa juzi ni kuona mkutano huo uliweza kufanyika na kwamba serikali ya Marekani iliuitia maanani mno.Kwsani, ni dola mbili kuu za ulimwengu wetu zilizokutana na marekani imetambua kuwa bila kuishirikisha China ,hakuna kinachoweza leo kutendeka.Huo ulikuwa mkutano wa dola 2 uso kwa uso."

Gazeti la Mannheimer Morgen linatuchukua katika siasa za ndani ya Ujerumani na kuchambua hatua ya jana ya waziri wa nje wa Ujerumani, Steinmeier -mtetezi wa ukanzela katika uchaguzi ujao na timu yake mpya:Laandika :

"Je, Bw.Steinmeier kweli anaonesha nguvu zake pale anapompiga kumbo mwanamke alieungama hatia yake na ambae muda mfupi kabla aliungwamkono na uongozi wa chama ?

Waziri huyo wa nje anabainika zaidi ni mtu anaesukumwa kuchukua hatua kutokana na hali ya kujikuta mashakani.Kumtimua nje ya timu yake Bibi ulla Schmidt (Waziri wa afya) ni kitendo cha kufadhahika.Bibi Schmidt asiamini kwamba atarejeshwa katika timu hiyo hata ikiwa tuhuma anazosukumiwa zikibainika kuwa kweli.Kwani, katika safari ya kuingia ikulu Berlin, gari la Mercedes chapa S-Klasse lisitumike tena.Sasa ni zamu ya gari la volkswagen."Laandika Mannheimer morgen.

Ama gazeti la Wiesbadner Kurier likiendeleza kisa hiki cha Bw.steinmeier-Ulla schmidt na SPD laandika:

"Pembe ya ya uongozi kwa baraza la mawaziri amekawia kuianzisha Bw.Steinmeier.Kwani sasa amepitwa na motokaa ya waziri wa afya Ulla schmidt.Timu ya kampeni ya uchaguzi ilipaswa kujiandaa kwa tokeo kama hilo.

Pengine, kutoka kashfa hii, yamkinika akapata nafuu-kwani inampa nafasi kuwachagua vijana zaidi na wanaowekewa tamaa badala ya wanasiasa wenye nguvu lakini siku zao zimekwisha."

Gazeti la DRESDNER NEUESTE NACHRICHTEN linachambua kurejea kwa bingwa wa zamani wa mbio za magari za FORMEL I,Michael Schumacher mashindanni baada ya kustaafu ili kuliokoa kampuni la motokaa la FERRARI. Laandika:

"Ferrari ilijikuta katika mashaka makubwa.Katika msimu huu mpya wa mbio za magari, Ferrari zilizowea kushinda, zimekuwa zikiburura mkia.Mwishoni mwa wiki iliopita, zilipatwa na mkosi wa ajali ya dereva wake Felipe Massa.Hapo tena vilio vya kumwita bingwa wa zamani, mjerumani Michael Schumacher vilihanikiza.Kurejea kwa Schumacher, kutazisisimua tena mbio za magari za Formel I...."

Mwandishi :Ali Ramadhan /Dt Zeitungen

Mhariri:M.Abdul-Rahman