1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA.Mwanamke wa Kipalestina auwawa na jeshi la Israel

Wanajeshi wa Israel wamefyatua risasi kuwaelekezea wanawake wa Kipalestina ambao walikuwa wamefanya ukuta wa kibinadamu kuwakinga wapiganaji wa Kipalestina walikuwamo ndani ya msikiti katika mji wa Beit Hanoun kaskazini mwa mji wa Gaza.

Katika shambulio hilo mwanamke mmoja wa kipalestina ameuwawa na wengine kumi wamejeruhiwa.

Hata hivyo takriban wapiganaji 60 wa Kipalestina waliokuwa ndani ya msikiti huo walifanikiwa kutoroka.

Msikiti huo ulikuwa uko chini ya ulinzi wa majeshi ya Israel tangu jana.

Waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniya amelaani operesheni hiyo ya majeshi ya Israel na kusema kuwa hatua hiyo ni ya kutekeleza mauaji ya umma wa Kipalestina.

Mwanajeshi mmoja wa Israel pia ameuwawa katika operesheni hiyo.

Takriban Wapalestina 20 wameuwawa tangu kuanza operesheni hiyo siku ya jumatano ambayo jeshi la israel inaaita operesheni ya kujibu mashambulio ya roketi yanayofanywa na wapiganaji wa Kipalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com