1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza.Israel yaendelea na maafa yake huko Gaza.

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvY

Mpalestina mmoja ameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya Israel kaskazini mwa ukanda wa Gaza katika kambi ya wakimbizi ya Jebaliya.

Mashahidi wamesema ndege za kijeshi za Israel zilikuwa zikiwatafuta kwa ajili ya kuwashambulia wanamgambo wa Kipalestina ambao walikimbia.

Jeshi la Israle limekuwa likifanya mashambulizi dhidi ya vikundi vya Kipalestina vinavyofanya mashambulizi ya maroketi huko katika mji wa Beit Hanoun na vile vile kaskazini mwa Gaza tangu wiki iliyopita.

Vikosi vya kijeshi vimeshawauwa Wapalestina 48 wengi wao wakiwa ni wanamgambo.