1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Hamas na Fatah wasitisha ghasia

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiX

Vyama vinavyopingana huko Palestina Hamas na Fatah vimekubaliana kusitisha ghasia katika eneo la ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa duru za habari pande hizo mbili zimeafikiana kukomesha mapigano yaliyozuka kwenye barabara za eneo hilo pamoja na kuwaondoa wanamgambo na kurejea katika mdahalo wa kitaifa juu ya kutafuta suluhu.

Kiasi cha watu watatu akiwemo msichana wa umri wa miaka 19 waliuwawa katika mapigano ya risasi kati ya chama cha Hamas na Fatah huko Gaza,mapigano ambayo yalizuka baada ya rais Mahmud Abbas kuitisha uchaguzi wa mapema jambo ambalo limepingwa vikali na chama cha Hamas kinachotawala Palestina.