GAZA: Wapalestina wanne wauwawa na jeshi la Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 14.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Wapalestina wanne wauwawa na jeshi la Israel

Wanajeshi wa Israel wamewaua wapalestina wanne wakati wa operesheni waliyoifanya leo kusini mashariki mwa Ukanda wa Gaza.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema uvamizi huo ulilenga kutafuta mtandao wa mahandaki unaotumiwa na wanamgambo wa kipalestina ili kuzuia maroketi kuvumishwa dhidi ya Israel.

Duru za hospitali zinasema mama mmoja pamoja na mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 25 wameuwawa na kombora la Israel wakati walipokuwa ndani ya nyumba yao.

Walioshuhudia wanasema watu wengine wasiopungua 11 wamejuruhiwa katika uvamizi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com