1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wapalestina 12 wauawa na wanajeshi wa Israel

28 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBni

Mashambulio yaliyofanywa na vikosi vya Israel katika Ukanda wa Gaza,yameua si chini ya Wapalestina 12,miongoni mwao wakiwemo raia pia. Wanajeshi wa Kiisraeli waliyosaidiwa na vifaru, walifyatuliana risasi na Wapalestina wenye silaha katika mji wa Gaza na mji wa kusini,Khan Younis. Maafisa wa majeshi ya Israel wamesema,wanasaka wanamgambo na silaha zitakazoweza kutumiwa kushambulia vituo vya Kiisraeli.