1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Viongozi wa Hamas waamuru zahati za kibinafsi zifungwe

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVO

Viongozi wa kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza wameamuru madaktari wanaofanya mgomo wafunge zahanati zao za kibinafsi leo katika changamoto mpya dhidi ya rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.

Mgogoro huo umekwamisha huduma za matibabu katika Ukanda wa Gaza hivyo kuzidi kuifanya hali ya kibinadamu kuwa mbaya katika eneo hilo.

Madaktari ambao hawatatii amri hiyo watafutwa kazi na zahanati zao zitachunguzwa kukahikikisha zimesajiliwa kwa njia ya halali na zimepewa leseni.