GAZA: Shule ya Umoja wa Mataifa yashambuliwa
7 Mei 2007Matangazo
Mtu mmoja ameuawa na wengine 6 wamejeruhiwa baada ya mtu mwenye bunduki kufyatua risasi katika shule inayoongozwa na Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza.Afisa mmoja amesema,washukiwa 3 wamekamatwa.Kwa mujibu wa maafisa,shambulio hilo lililofanywa na wafuasi wa kundi lenye itikadi kali za kidini,lililenga sherehe ya michezo ya spoti ya shule hiyo,iliyohudhuriwa na wasichana na wavulana.