1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza - Israel yaenmdelea kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Gaza.

Eric Kalume Ponda19 Januari 2009

Baada ya Israel kutangaza hatua ya kusimamisha mapigano na wafuasi wa chama Hamas, milolongo ya vifaru vya jeshi la Israel vilivyoingia eneo hilo Januari 3 vyarejea nyumbani Israel.

https://p.dw.com/p/GcCl
Wanajeshi wa Israel wakiwa juu ya vifaru kuondoka GazaPicha: picture alliance / landov


Hali hiyo imetoa nafuu kwa raia wa Gaza ambao waliendelea kuondoa vifusi huku idadi ya watu waliofariki ikiongezeka baada ya maiti zaidi kupatikana katika vifusi hivyo. Hata hivyo bado kuna hali ya wasi wasi nini kitakachofuatia baada ya muda wa wiki moja uliotangazwa na Hamas kumalizika.


Hofu hiyo inatokana na kwamba wafuasi wa chama cha Hamas wanatambua muafaka huo kwa muda wa wiki moja pekee, huku wakisisitiza kuwa masharti yao ni lazima yatimizwe kabla ya kuafikiwa mkataba kamili wa kumoesha mapiganio na kudumisha amani katika eneo hilo la Ukanda wa Gaza.


Wajumbe kwenye mpango wa amani unaoongozwa na misri walitia saini makubaliano na maafisa wa Israel kuhusu mpango wa kusimamiwa kwa maeneo ya mpakani yasijetumiwa na wafuasi wa Hamas kuingiza silaha kimeganedo.


Chama cha Hamas hakikushiriki kwenye mazungumzo hayo kwani kinasisitiza kuwa maeneo yote ya mpakani lazima yafunguliwe na kuondoka kabisa kwa jeshi la Israel katika ardhi ya Gaza.


Israel inasema kuwa shughuli ya kuwaondoa wanajeshi kutoka Gaza huenda ikamalizika Jumanne ijayo. Katika makubaliano ya leo, Misri imetoa hakikisho kwa Israel kwamba itachukua kali katika kusimamia maeneo yote ya mpakani.


Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert alisema kuwa nchi yake inataka kusimamia maeneo hayo ili kuhakikisha ni vyakula pekee na misada mingine ya kibinadamu inayoingiza Gaza.

alisema Bw Olmert..``nataka kutoa wito kwa raia wa Gaza. Mara kwa mara ninapozungumzia suala hili, kujaribu kuwasihi na kuwaeleza, ni lazima mfahamu kuwa adui wenu si Israel, ni Hamas ndio adui wenu mkubwa na makundi ya kigaidi. Kwa hakika hatukutaka kuwasababishia mateso rais wa Gaza. Tunasikitishwa na idadi ya watu waliofariki na kwa niaba ya seriikali ya Israel naomba msamaha kwa watu wasio na hatia walioathirika na oparesheni hii´´.


Kwa mara ya kwanza tangu vita hivyo vianze chama cha Hamas kimetoa idadi ya wapiganaji wake waliouawa kuwa wafuasi wake 48 wakati wa mashambulio hayo na kinasisitiza kuwa kimepata ushindi mkubwa katika vita hivyo.


Baada ya Serikali Israel kutoa tangazo ya kusimamisha mapigano, sasa juhudi zinaeelekezwa katika ujenzi wa eneo hilo, ambapo tayari mataifa kadhaa yameahidi kutoa mchango wake ikiwa Saudi Arabia ambayo imeahidi kiasi cha dola bilioni 1.


Afisa mwakilishi wa umoja wa mataifa ya Ulaya Benita Ferrero alisema hata hivyo kwamba Umoja wa Ulaya hautashiriki katika shughuli za ujenzi wa eneo hilo hadi pale wafuasi wa Hamas watakapokomesha mashambulizi ya mizinga ya Maroketi dhidi ya Israel.


Ripoti ya hivi punde inasema kuwa maiti 100 zaidi zimeondolewa kutoka vifusi vya majengo yaliyobomolewa katika eneo hilo kufuatia mashambulizi hayo yaliyodumu kwa siku 22. Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya nyumba 20,000 za makaazi, majengo 16, misikiti 20 na majengo mengine 5,000 yameharibiwa kabisa.

Shughuli za ujenzi mpya ikiwa ni pamoja na miundo katika eneo hilo zinatarajiwa kugharimu kiasi cha dola bilioni 2.


Ponda/Afp..