1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G-8 na China

23 Mei 2007

China inaongoza duniani kwa kuigiza bidhaa za nchi na makampuni mengine .Inatuhumiwa kukiuka haki-miliki na vitambulisho vya bidhaa.

https://p.dw.com/p/CHDu
Basi ya aina ya Kijerumani inayojengwa na Wachina bila ya ruhusu
Basi ya aina ya Kijerumani inayojengwa na Wachina bila ya ruhusuPicha: AP/NEOMAN Bus

Haki-miliki ni mojawapo ya mada zitakazojadiliwa katika mkutano ujao wa kilele wa kundi la dola kuu 8 tajiri ulimwenguni-G-8 mjini Heiligendamm,Ujerumani.China imekuwa ikigonga vichwa vya habari kwa kuigiza bidhaa zinazotengezwa na nchi nyengine au kwiba ufundi na ujuzi wa wengine.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani,mwenyekiti wakati huu wa mkutano huo wa G-8 na halkadhalika, Rais wa Umoja wa Ulaya wakati huu, amejitolea kulinda haki-miliki na kuifanya mada hiyo kuwa usoni katika kikao hicho.

Swali hili si ajabu kuangukia katika ajenda ya mkutano ujao wa kilele wa dola kuu 8 tajiri:Kwani mtindo wa kuigiza bidhaa za mwenzako na vitambulisho vya bidhaa zake unasababisha hasara kubwa katika uchumi ipatayo Euro bilioni 300.

Mabingwa wa dunia katika mtindo huo ni Jamhuri ya Watu wa china ,kwani kiasi cha nusu ya bidhaa za kuigiza zinazokamatwa na Idara za forodha na polisi na wizi wa haki-miliki zinatoka China.

Swali je, hii ni tabia ya Asia au serikali ya China inalifumbia macho tatizo hili huku viwanda na makampuni yake vikizalisha bidhaa kama hizo haraka mno na kwa bei nafuu na kuziuza na kuigiza ufundi wa kimamboleo wa wengine?

Viwanda vya kutengezea mashini vya Ujerumani vinastawi wakati huu kutokana na kutakiwa m,no zana zake na China.Maagizo ya China ya mashini na ufundi wa kisasa kabisa wa Ujerumani iliongezeka kwa kima cha 16% hapo 2006.Kwahivyo, China imekuwa soko la pili kwa ukubwa katika sekta hii ya machine za Ujerumani duniani.Kwa bahati mbaya hata peni hili lina sura mbili asema Dieter Bruclacher,rais wa Shirika la viwanda vya mashini vya Ujerumani VDMA:

“Mafanikio ya bidhaa zetu yaongoza pia kuigizwa.Hii imeoneshwa na uchunguzi wa shirika letu uliofanywa mwezi Machi mwaka huu kuwa wizi wa bidhaya kwa n jia ya kuigiza umeongezeka mno.Imegunduliwa 75% ya visa vya aina hivyo China imehusika.”

Serikali kuu mjini Beijing ikijaribu tangu kupita miaka mingikubadili hali hii alao kidogo bila kufanikiwa.Kwa kufungua milango ya soko lake mwishoni mwa 1970,China ilianza pia kujenga taasisi za kisheria kulinda haki-miliki.Sheria ziliopo sasa za kulinda haki-miliki ,alama za bidhaa na haki miliki zalingana na daraja zinazotakiwa na shirika la biashara duniani (WTO).

Tatizo lipo katika kutekeleza sheria hizo adai prof. Robert Heuser wa chuo kikuu cha Cologne:

“Serikali zas kienyeji hazijali kulinda haki-miliki na mashtaka mbele ya mahkama za mikoa hiyo hayana maana yoyote kwavile, mahakma huko zinazitegemea mno serikali hizo za kienyeji.”

Mbali na matatizo yake ya miundo-mbinu,mabingwa wa China hapa Ujerumani wanajaribu kujipatia jibu la tatizo hilo katika mila na utamaduni wan chi za Asia.

Kwani tayari tangu mwaka 25000 taaluma ya konfuzius ilifunza kuwa: Yule anaemuiga bingwa ,huwa ndio amtukuza.”Katika karne ya 7 wataalamu wa kichina wakafunga safari hadi India ili kuigiza dini ya Budha.Kwahivyo, mchina ni mtu anaeigiza kutokana na mila ?”

Duan Guijian,mkurugenzi wa taasisi ya kulinda haki miliki nchini China anaeleza kwamba, katika karne ya 15 na 16,mji wa Venice ndio uliokua shina la biashara barani Ulaya.Kuporomoka kwa Venice kulichangiwa na tangu sababu za kisiasa hata za kiuchumi.Bidhaa bandia zilianza kumiminka huko Venice kutoka sehemu nyengine za Ulaya.

Venice ilikua imesheheni bidhaa bandi .nini chanzo chake ? Je, ilitokana hii na mila na desturi za kikristu ?

Sababu za kukiukwa haki-miliki nchini China aona Duan Gujian, kunatokana na utaratibu wa maguezi ya uchumi wa China.