1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

FINALI YA KOMBE LA FA:MANCHESTER NA CHELSEA

Wakati katika Bundesliga,Schalke imen'gan'gamnia nafasi ya kwanza kileleni ,huko Uingereza Chelsea imepanga miadi na Manchester united katika finali ya kombe la FA.

Timu zote 4 kileleni mwa Bundesliga zilitamba tena kwa wiki ya pili mfululizo na hivyo, sio tu zimetilia kasi kinyan’ganyiro cha ubingwa bali hata kile cha kuania nafasi 2 za kucheza champions-League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.

Viongozi wa Ligi Schalke, waliizaba Mainz mabao 3:0.Alikua tena Kevin Kuranyi, alieufumania kwanza mlango wa Mainz mnamo dakika ya 10 ya mchezo kabla hakumtupia pasi maridadi Gerald Asamoah kwa bao la pili.

Halafu Lincol alierejea uwanjani baada ya kufungiwa kucheza mapambano 5 alilipiza kisasi kwa kutia bao la 3 la Schalke.

Sasa Schalke, ambayo haikuwahi kutwaa ubingwa tangu 1959 ilipounyakua kwa mara ya 7 na ya mwisho,imekusanya sasa jumla ya pointi 59 na inafuatwa na Wrder Bremen ilio nyuma kwa pointi 2 huku Stuttgart ikiwa pointi 2 nyuma ya Bremen.Munich, mabingwa wananyatia nafasi ya 4 kwa pointi 53.

Hapo kabla Schalke ilikuwa kwake kufa-kupona katika changamoto yake na mainz inayopigana isirejee daraja ya pili msimu ujao.Kwani, wangeteleza basi Bremen ikishika usukani wa Ligi.

Akielezea ushindi huo ulikujaje kocha wa Schalke Klonska alisema:

“sisi ni Schalke 04 wala sio Bayern munich.Timu yangu imetekeleza mkakati wake barabara na kwa werevu mno.Na hiyo ndio sifa kwa timu iliopo kileleni kuionesha na ndio maana tuko kileleni hjivi sasa.Wakati wote tulikua macho nah ii ni muhimu ukipambana na Mainz.”

Finali ya kwanza kabisa ya Kombe la FA la Uingereza katika uwanja mpya wa Wembley,mjini London itakua jumamosi ijayo kati ya Chelsea na Manchester united .Kwani zote 2 zilitamba katika nusu-finali mwishoni mwa wiki.

Manchester ilikomea Watford mabao 4-1 huku Wayne Rooney akilifumania lango la Watford mara mbili.Chelsea ilihitaji kurtefushwa mchezo na balo la mjerumani Michael ballack kuizika Blackburn iliotoa changamoto kali kabisa kabla kusalim amri.

Huko Itali,Inter Milan ilipunguza mwanya wake hadi ushindi mmoja kabla haikutawa tena taji la Itali kwa mwaka wapili mfululiuzo.Inter ilitoka nyuma na kuondoka suluhu na Palermo.AC Milan mahasimu wa mtaani wa Inter waliikomea Messina 3-1 kufuatia mabao maridadi ya Kaka,Favalli na Ronaldo.

Huko Spain mabingwa FC Barcelona waliendeleza ushindi wao kileleni mwa La Liga kwa pointi 4.Ushindi wao mwishoni mwa wiki lakini ulikuja dakika za mwisho kwa bao la Navarro dhidi ya Real Mallorca.

Huko Ufaransa, Olympique Lyon iko pia ushindi mmoja tu mbali na kuvaa tena taji la ubingwa tena kwa mwaka 6 mfululizo.

Katika dimba la michezo ijayo ya bara la Afrika-All-Africa Games huko Algiers, mabingwa simba wa nyika-Kameroun ilitimua Gabon kwa mabao 5:0.

Sasa simba wanyika wamepanga miadi na Ghana,Bafana Bafana-au Afrika Kusini na Tunisia.Changamoto zitachezwa Algeria kati ya Julai 11 na 23.

Rais wa FIFA-shirikisho la kabumbu ulimwenguni Sepp Blatter ameitaka leo India yenye wazimu wa mchezo wa cricket kugeukia zaidi dimba akidai kwamba kabumbu laweza likawatia wazimu hata mkubwa zaidi wahindi kuliko cricket kutokana na idadi kubwa ya wakaazi wake bilioni 1.

Blatter aliwaambia mripota wakati wa ziara yake ya kwanza rasmi nchini India.India wakati huu inasimama nafasi ya 165 katika ngazi ya dunia na 34 katika orodha ya timu za dimba barani Asia.

 • Tarehe 16.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcM
 • Tarehe 16.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcM