Fidia za migodi ya makaa kukoma na mabishano ya hali hewa: | Magazetini | DW | 30.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Fidia za migodi ya makaa kukoma na mabishano ya hali hewa:

Hizo ndizo mada mbili zilizowashughulisha mno wahariri wa magazeti yaliotoka leo Ujerumani:

Serikali ya shirikisho na zile za mikoa ,viwanda na vyama vya wafanyikazi, zimekubaliana kimsingi,kuachana na kulipia fidia migodi ya makaa yam awe baada ya 2018.

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG laandika:

„…….Hii ni habari nzuri,lakini kwamba itapita miaka11 yaani hadi 2018 kusimamisha fidia hiyo,ni labari mbaya.Kwani hadi wakati huo,mlipaji kodi humu nchini atakuwa ameshachangia Euro bilioni 30 kulipia fidia za migodi hiyo ya makaa ya mawe na hii maana yake ni kuendelea kupoteza pesa za bure.“

Ama kwa gazeti la AACHENER ZEITUNG uamuzi huo uliokatwa una maana pia kuachana kabisa na mila na desturi ndefu ya chama cha kijamaa cha SPD.

Laandika kwa chama cha SPD hii maana yake kubadili msimamo wake kuelekea kuizika kabisa migodi ya makaa ya mawe na hii lazima ni shubiri na ngumu kwa chama hiki,kwani ni enzi mpya.

Kwani, hakuna mada nyengine ilioshikamana mno na roho ya chama cha kijamaa cha SPD kama migodi hiyo na wafanyikazi wake wanaotokwa na jasho kwenye mashimo hayo ya makaa ya mawe.

Ama BADISCHE TAGBLATT kutoka Baden-Baden linasema kwa dhihaka kwamba:

Katika uchimbaji makaa ya mawe sasa imeamuliwa „bora sasa kukomesha uchimbaji na kuvumilia uchungu kuliko uchungu usio na mwisho wake.

Muafaka wowote ule wa kisiasa ambao utarefusha bila kuhitajika ulipaji fidia kwa migodi hiyo,kutagharimu tu mabilioni zaidi.“

Katika gazeti la LANDESZEITUNG kutoka Lüneburg tunasoma:

„Viwanda na wanasiasa wamekubaliana maziko ya hadhi ya juu kabisa ya migodi ya makaa ya mawe.Moja ni wazi maziko hayo yalikuwa yafanyike kitambo sana.

Kwani kitambo sana migodi hiyo ya dhahabu iligeuka migodi ya kufadhiliwa na fidia tena bila sababu.Fedha hizo zingeweza kutumiwa vyema zaidi ,kwa mfano katika kukuza nishati ya kutumika tena na tena…..Mwaka 2012 mpango huu wa kuachana na migodi ya makaa ya mawe utadurusiwa tena iwapo ni sawa au la.Hii ni busara.

Likitugeuzia mada ,gazeti la FRANKFURTER NEUE PRESSE linajishughulisha na mvutano uliozuka baina ya UU na serikali ya Ujerumani kuhusu kuchukua hatua kali zaidi kuhifadhi mazingira.Gazeti laandika:

„ Wajerumani hawana sababu kuwanyoshea wenzao kidole.Ndio hisia za kulinda mazingira zimemjaa kila mmoja nchini Ujerumani na Ujerumani ndio inayoongoza katika kusaka njia nyengine za nishati inayoweza kutumika tena.

Lakini, hatua kali zisopendwa kama vile kulazimisha kikomo maalumu cha mwendo wa magari,

ili kupunguza moshi unaopaa hewani kuchafua mazingira ,hazipendwi Ujerumani.Isitoshe, wanasiasa nao hawamudu kulazimisha vipimo maalumu visikiukwe vya gesi kwa kuchelea kuyaudhi makampuni ya uundaji magari.“

Nalo OSTTHÜRINGER ZEITUNG kutoka Gera, linazungumzia mvutano ndani ya serikali ya muungano ya Ujerumani kuhusu vipimo vya moshi wa magari.Laandika:

„ waziri wa uchumi Bw.Glos amejiweka upande wa wanaviwanda wa magari wanaolalamika wakati waziri wa mazingira Bw.Gabriel asema Bw.Glos anabidi kwanza kuangalia mkataba uliounda maafikiano ya serikali yao ya muungano .Katika mkataba huo vipimo vya gesi inayochafua mazingira vilikwishafikiwa na yeye alichangia.“