1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dresden:Taka za nuklea zarudishwa Urusi

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiU
Mwanamke wa Kisomali akipita katika eneo lililoharibiwa kwa makombora mjini Mogadishu.
Mwanamke wa Kisomali akipita katika eneo lililoharibiwa kwa makombora mjini Mogadishu.Picha: picture-alliance/ dpa

Kiasi ya kilo 300 mabaki ya miale ya sumu kutoka kinu cha utafiti wakati wa enzi ya Urusi ya zamani, zinasafirishwa kwa ndege kutoka Ujerumani kupelekwa Urusi. Urutubishaji wa uranium utafanywa nchini humo chini ya mkataba wa kimataifa unaofafanua kwamba zana zozote za kinuklea za wakati wa vita baridi zirejeshwe katika nchi ya asili. Taka hizo zilitokana na kinu cha utafiti wa kinuklea katika mji wa Rossendorf karibu na Dresden katika iliokua zamani Ujerumani mashariki. Kinu hicho kilifungwa mwaka 1991. Wataalamu wamesema kuna usalama kuisafirisha kwa ndege uranium iliorutubishwa, kuliko kwa treni. Usafirishaji wa taka hizo hadi uwanja wa ndege, ulizuiwa kwa muda na kundi la wapinzani wa matumizi ya nuklea.