DAR ES SALAAM:Benki ya Dunia yatoa dola milioni 60 kupambana na malaria | Habari za Ulimwengu | DW | 06.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DAR ES SALAAM:Benki ya Dunia yatoa dola milioni 60 kupambana na malaria

Benki ya Dunia imeidhinisha msaada wa dola milioni 60 ili kusaidia nchi ya Tanzania kupambana na malaria vilevile kugharamia mafunzo ya wafanyikazi wa huduma za afya katika maeneo ya vijijini.

Kulingana na benki hiyo dola milioni 25 zitatumika kununulia vyandarua vya mbu vilivyotiwa dawa kupunguza ueneaji wa malaria.Dola milioni 35 zilizosalia zitatumika kutoa mafunzo kwa wafanyikazi wa huduma za afya katika mabaraza 121 ya wilaya.

Nchi ya Tanzania ina wakazi milioni 40.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com