1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Mkutano kati ya Hamas na Fatah waahirishwa mjini Damascus, Syria.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZ6

Mkutano uliopangwa kati ya Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, na kiongozi wa chama cha Hamas, Khalid Mashaal, umeahirishwa baada ya wasaidizi wa viongozi hao kushindwa kutatua tofauti zilizopo kuhusu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Mkutano huo ulipangwa kufanyiwa mjini Damascus ambako Khalid Mashaal anaishi uhamishoni.

Duru zinasema chama cha Hamas na chama cha Fatah kinachoongozwa na Mahmoud Abbas, bado havijakubaliana kuhusu masuala kadhaa, likiwemo suala la kuundwa baraza la mawaziri.