1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY: Hali ya hatari yatangazwa

13 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSl

Rais Lansana Conte wa Guinea ametangaza hali ya hatari nchini mwake na kuyaamuru majeshi ya nchi hiyo yarejeshe hali ya utulivu baada ya kuzuka vurugu dhidi ya serikali yake.

Takriban raia tisa waliuwawa katika mji mkuu wa Conakry baada ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuitisha mgomo kupinga uamuzi wa rais Conte wa kumchaguwa rafiki yake wa karibu Eugene Camara kuchukuwa wadhfa wa uwaziri mkuu.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanadai kuwa rais Conte mwenye umri wa miaka 72 hastahiki kuingoza nchi ya Guinea baada ya kukaa madarakani kwa miongo miwili mfululizo.